Admissions | KOWAK

Jinsi ya kujiunga na shule yetu

Unaweza kupakua fomu hiyo kwenye mtandao wetu huu kwa gharama ya TSh 15,000/=

Maelekezo ya kununua fomu mtandaoni

  1. Lipia TSh 15,000/= kwenye namba ifuatayo
    0744 656 706 
    Jina: KOWAK SECONDARY SCHOOL
    Tumia namba ya simu kufanya malipo. Usiweke pesa kwa wakala wala kuhamisha toka benki kuja kwetu moja kwa moja.
    Ukitumia wakala / benki hatutapata namba ya simu iliyofanya malipo hivyo mifumo yetu haitaweza kushughulikia muamala wako
  2. Ndani ya muda mfupi tutakutumia ujumbe kwenye namba uliyoitumia kufanya malipo. Ujumbe huo utakuwa na token.
  3. Bonyeza Pakua fomu. Ingiza namba ya simu uliyotumia kufanya malipo.
  4. Ingiza token tuliyokutumia kwa ujumbe mfupi
  5. Ingiza majina mawili ya mwanafunzi kwenye sehemu husika, kama alivyosajiliwa kwenye mtihani wa darasa la saba.
  6. Chagua lugha atakayoitumia mwanafunzi kufanya mtihani wa kuingia. Iwapo mwanafunzi amemaliza darasa la saba kwenye shule ya English Medium chagua English. La sivyo chagua Kiswahili.
  7. Hakiki jina la mwanafunzi na lugha. Hutaweza kubadilisha baada ya hatua hii. Kama ni sawa bonyeza Hifadhi Taarifa
  8. Pakua fomu. Ichape na ufuate maelekezo yake.